Simba Sports Club
News

Tumepangwa Kundi C Mapinduzi Cup

23 Dec 2021 By simbasc 1,422 views

Ratiba ya Michuano ya Mapinduzi Cup ambayo hufanyika Januari kila mwaka Visiwani Zanzibar imetoka na tumepangwa Kundi C.

Katika kundi letu zipo timu tatu tukiwa pamoja na Mlandege na Selem View.

Advertisement

Kwa mujibu wa ratiba kikosi chetu kitaanza kampeni hiyo kwa kucheza na Selem View Januari 5 katika Uwanja wa Amani saa 10:15 jioni.

Mchezo wetu wa pili utakuwa Januari 7 dhidi ya Mlendege ambao utafanyika Uwanja wa Amani saa 2:15 usiku.

Back to homepage
Share this story