Balua ambaye ana uwezo wa kucheza winga zote au nyuma ya mshambuliaji (namba 10) amekuwa akijitajika na timu hiyo kwa muda mrefu hivyo kwa manufaa yake binafsi, klabu pamoja na nchi tumemruhusu kwenda kujiunga nao.
Klabu ya Simba inaamini katika kipindi cha mwaka mmoja ambacho Balua atakachokuwa nchini Cyprus itamuongezea vitu tofauti ambavyo vitakuwa msaada mkubwa katika maisha yake ya soka.
Advertisement
Tumekuwa na utaratibu wa kuruhusu wachezaji wetu kujiunga na klabu zinazowahitaji hasa za Kimataifa kila wanapohitajika ikiwa ni kwa manufaa yao, Klabu na Taifa kwa ujumla.
Simba inamtakia kheri Balua katika kipindi chote atakachokuwa katika klabu yake mpya Enosis Neon Paralimni FC