Simba Sports Club
News

Tumemaliza Mzunguko wa kwanza TWPL tukiwa kileleni

17 Feb 2024 By simbasc 376 views
Mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL) umemalizika huku kikosi cha Simba Queens kikiwa kileleni mwa msimamo. Ligi ya Wanawake ambayo inashirikisha timu 10 imesimama kupisha maandalizi ya timu ya Taifa ya Twiga Stars kujiandaa na michuano ya kufuzu Olimpiki dhidi ya Afrika Kusini 'Banyana Banyana'. Simba Queens imemaliza mzunguko huo ikiwa na alama 25 baada ya kucheza mechi tisa ikishinda nane na kutoka sare moja. Katika michezo hiyo Queens imefunga mabao 33 huku ikiruhusu kufungwa mabao matano. Matokeo ya mechi zote tisa za Simba Queens Simba Queens 5 - 0 Ceassia Queens Simba Queens 5 - 2 baobab queens Simba Queens 3 - 1 Yanga Princess Simba Queens 3 - 0 JKT Queens Amani Queens 2 - 3 Simba Queens Bunda Queens 0 - 0 Simba Queens Simba Queens 7 - 0 Alliance Girls Fountain Gate Princess 0 - 4 Simba Queens Geita Queens 0-3 Simba Queens
Advertisement
Back to homepage
Share this story