Simba Sports Club
News

Tumemaliza Mzunguko wa kwanza Kibabe

28 Dec 2024

Tulianza mchezo kwa kasi huku tukifika zaidi langoni mwa Singida lakini mashambulizi yetu yaliishia kwa walinzi pamoja na mlinda mlango, Metacha Mnata.

Fabrice Ngoma alitupatia bao hilo pekee dakika ya 41 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Jean Charles Ahoua.

Kipindi cha pili kasi ya mchezo iliongezeka huku Singida nao wakifika langoni kwetu mara kadhaa lakini mlinda mlango Moussa Camara alikuwa imara.

Ushindi huo umetufanya kufikisha pointi 40 tukiwa kileleni mwa msimamo baada ya kucheza mechi 15.

Advertisement

X1: Metacha, Ande, Imoro (Manyama 63'), Kennedy, Trabi, Damaro, Khalid (Adebayor 75'), Keyekeh, Arthur, Tchakei (Lyanga 63'), Rupia

Walioonyeshwa kadi: Tchakei 18' Imoro 21' Kennedy 58'

X1: Camara, Kapombe, Zimbwe Jr (Chamou 70'), Hamza, Che Malone, Kagoma, Kibu, Ngoma, Mukwala (Ateba 90') Mpanzu (Awesu 70'), Ahoua (Fernandez 80')

Walioonyeshwa kadi: Kagoma 65'

Back to homepage
Share this story