Pesa hizo ni motisha inayotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa timu za Tanzania zinazoshiriki michuano ya Kimataifa.
Akizungumza wakati wa kukabidhi pesa hizo Dkt. Ndumbaro amekipongeza kikosi chetu kwa ushindi huo lakini akitusisitiza kuendelea na maandalizi kwa ajili ya mechi nyingine zinazofuata.
Advertisement
"Hongereni Simba kwa kuibuka na ushindi huu wa leo, sote tumeona haikuwa kazi rahisi na mara zote Rais wetu Dkt. Samia amekuwa akifurahi kuona wanamichezo wa Tanzania wakifanya vizuri kimataifa," amesema Dkt. Ndumbaro.