Simba Sports Club
News

Tumeibuka na ushindi dhidi ya Al-Adalah

29 Jul 2024

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku timu zikishambuliana kwa zamu ambapo mshambuliaji Steven Mukwala alitupatia bao mapema dakika ya tisa baada ya kumalizia pasi safi iliyopigwa na Fabrice Ngoma.

Joshua Mutale alitupatia bao la pili dakika ya 32 baada ya kupokea pasi kutoka Ngoma tena.

Kipindi cha pili Al- Adalah walirudi kwa kasi na walifanikiwa kupata penati baada ya kipa Ally Salim kufanya madhambi ndani ya 18.

Advertisement

Kocha Fadlu Davids alifanya mabadiliko ya kuwatoa Mukwala, Mzamiru Yassin, Edwin Balua, Shomari Kapombe na kuwaingiza Valentino Mashaka, Awesu Awesu, Augustine Okajepha na Kelvin Kijili.

Mchezo wa leo ni wa mwisho kwa kirafiki hapa Misri kabla ya kuanza safari ya kurejea nyumbani tayari kwa Tamasha kubwa la kihistoria la Simba Day.

Back to homepage
Share this story