Baada ya kupokea zawadi hiyo, Farik ameushukuru uongozi wa klabu kwa kuonyesha mshikamano huku akisisitiza anaomba usiishie hapa bali uendelee.
"Tunawashukuru kwa ushirikiano mkubwa mliotupatia, tumefurahi kwa zawadi na tunaamini urafiki huu utaendelea baada ya hapa," amesema Farik.
Advertisement
Al Hilal walitualika kushiriki michuano maalum kwa ajili ya kuandaa timu zetu kuelekea Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika michuano ambayo Timu ya Asante Kotoko ya Ghana ilishiriki.