Simba Sports Club
News

Tumegawana pointi na Polisi

10 Apr 2022

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku tukishambuliana kwa zamu lakini changamoto ikawa kumalizia nafasi zilizopatikana.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi na kutengeneza nafasi kadhaa huku wenyeji Polisi wakicheza kwa kuzuia zaidi na kufanya mashambulizi ya kushtukiza.

Advertisement

Kocha Pablo Franco aliwatoa Yusuf Mhilu, Mzamiru Yassin, Medie Kagere, Rally Bwalya na Erasto Nyoni na kuwaingiza Pape Sakho, Jonas Mkude, Clatous Chama, Bernard Morrison na Jimmyson. Mwanuke.

Matokeo haya yanatufanya kufikisha pointi 41 tukiwa nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 19.

Back to homepage
Share this story