Simba Sports Club
News

Tumegawana Pointi Kaitaba

12 May 2024

Mshambuliaji Freddy Michael alipoteza nafasi ya wazi dakika ya pili kufuatia kushindwa kumalizia pasi iliyopigwa na Mzamiru Yassin.

Ladaki Chasambi alitupatia bao la kwanza dakika ya 24 kwa shuti kali la chini chini baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na nahodha Mohamed Hussein kuzuiwa kwa kichwa na Sadio Kanoute.

Kipindi cha pili Kagera waliongeza kasi na kufanya mashambulizi mengi langoni mwetu huku wakirudi wote tunapo washambulia.

Obrey Chirwa aliisawazishia Kagera bao hilo dakika ya 61 baada ya kumalizia pasi ya Deus Bukenya kufuatia mpira wa kona ya chini chini iliyopigwa na David Luhende.

Advertisement

X1: Ngereka, Mhilu, Luhende, Duah, Bukenya, Seseme, Mbaraka, Manyasi, Chirwa, Amza, Galiwango (Mafie 45')

Walioonyeshwa kadi: Duah 30' Galiwango 37'

X1: Lakred, Israel, Zimbwe Jr, Kennedy, Che Malone, Babacar (Onana 77'), Balua (Jobe 87') Mzamiru Freddy, Kanoute, Chasambi

Walioonyeshwa kadi:

Back to homepage
Share this story