Simba Sports Club
News

Tumegawana alama na TRA Sheikh Amri Abeid

9 Apr 2026

Mchezo ulianza kwa kasi ya kawaida huku timu zote zikitengeneza nafasi chache huku mpira ukichezwa zaidi katikakati ya uwanja katika dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kufika zaidi langoni mwa TRA na kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini hata hivyo hatukuweza kuzitumia vema.

Matokeo haya yanatufanya kufikisha alama 36 tukiendelea kusalia nafasi ya pili kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 16.

X1: Noel, Isaack (Lazarus 76')Nouma, Tebandeke, Kombo, Jamal, Chobwedo, Chewe, Mugoya (Akandanwao 64'), Ng'anzi, Jiah (Mapaka 45')

Advertisement

Waliionyeshwa kadi: Nouma 81' 85 (nyekundu)

X1: Kassali, Kapombe (Duchu 85'), Kibabage, Toure, De Reuck, Kagoma, Gueye (Morice 61'), Kante (Chama 61'), Mwalimu (Mbegu 85') Maema (Loemba 76'), Oura

Waliionyeshwa kadi: Kibabage 63'

Back to homepage
Share this story