Simba Sports Club
News

Tumegawana alama na Petro De Luanda

7 Feb 2026

Mchezo ulianza kwa kasi huku tukishambuliana kwa zamu na nafasi zikitengezwa pande zote ingawa hazikutumiwa ipasavyo.

Pedro Pinto aliipatia Petro bao la kwanza kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa kichwa uliopigwa na Pereira.

Nahodha Shomari Kapombe alitolewa kwa kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 40 baada ya kumchezea madhambi mchezaji wa Petro.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi baada ya kufanya mabadiliko ya kuwaingiza Anicet Oura, Inno Loemba na Seleman Mwalimu ambao waliongeza ufanisi katika idara ya ushambuliaji.

Anicet Oura alitupatia bao la kusawazisha dakika ya 80 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Seleman Mwalimu.

Advertisement

X1: Hugo, Toro, Costinha, Benny, Pinto, Pereira, Reis, Kinito, Eddie, Hossi, Ilidio

Waliionyeshwa kadi: Kinito 72'

X1: Kassali, Kapombe, Mligo (Naby 78'), De Reuck, Toure, Kagoma, Morice (Duchu 44'), Kante (Loemba 51') Kibu (Mwalimu 51'), Chama, Mpanzu (Ouara 51')

Waliionyeshwa kadi: Kapombe 19' 40'

Back to homepage
Share this story