Simba Sports Club
News

Tumegawana Alama na Pamba CCM Kirumba

19 Mar 2026

Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu lakini mpira ukuchezwa zaidi katikati ya uwanjani safu zote za ulinzi zikiwa imara.

Anicet Oura alitupatia bao la kwanza dakika ya 33 akiwa ndani ya 18 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Elie Mpanzu.

James Mwashinga aliwapatia Pamba bao la kusawazisha dakika ya 35 kwa shuti kali la mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja baada ya kumshinda mlinda mlango, Djibrilla Kassali.

Kipindi cha pili timu zote zilirudi kwa kasi huku zikishambuliana kwa zamu ingawa nafasi zilizopatikana zikishindwa kutumiwa vema.

Matokeo haya yanatufanya kufikisha alama 28 tukiendelea kusalia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kucheza mechi 13.

Advertisement

X1: Amosi, Kunambi, Abraham, Mangalo, Mwashinga, Samamba (Eshiamba 71'), Zabona (Nakibinge 55'), Siwa (Nahimana 82'), Tegisi, Lwasa (Camara 71'), Kibailo

Waliionyeshwa kadi: Siwa 73' Amosi 90'

X1: Kassali, Kapombe Mligo, Toure, De Reuck (Mbegu 84') Kagoma, Gueye (Maema 84'), Kante (Morice 74'), Mpanzu, Chama, Oura

Waliionyeshwa kadi: Kagoma 81'

Back to homepage
Share this story