Elie Mpanzu alitupatia bao la kwanza dakika ya 19 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na nahodha, Shomari Kapombe akiwa ndani ya 18.
Baada ya bao hilo tuliendelea kulisogelea lango la Mtibwa na kufanya mashambulizi kadhaa lakini hata hivyo ufanisi wa kutumia nafasi tulizopata ulikuwa mdogo.
Magata Charles aliwapatia Mtibwa bao la kusawazisha dakika ya 60 kwa shuti kali nje ya 18 baada ya kupokea pasi kutoka Kassim Shaibu
Baada ya bao hilo timu zote zilishambuliana kwa zamu huku tukifika zaidi langoni mwa Mtibwa lakini hata hivyo matokeo hayakubadilika.
X1: Abel, Kapombe, Mligo (Morice 74') Nangu, De Reuck, Kagoma, Bajaber (Kibu 11' Mutale 63'), Naby, Mwalimu (Mukwala 63'), Maema (Masinde 74'), Mpanzu
Waliionyeshwa kadi: Kapombe 79'
X1: Victor, Costa, Lyawatwa, Magata, Datius, Mwashilindi (Chota 60'), Chicharo, Mkopi (Mhesa 82') Manga (Fabian 82'), Simchimba (Marungu 45'), Kassim (Nyangi 89')
Waliionyeshwa kadi: Datius 32' Costa 87'