Katika mchezo huo uliokuwa mkali muda wote tulipata bao la kwanza dakika ya tatu kupitia kwa kinara Aisha Mnuka ambaye alimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Ritticia Nabbosa.
Elizabeth wambui alitupatia bao la pili kwa shuti kali baada ya kupokea pasi safi iliyopigwa na Aisha Juma.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku tukishambuliana kwa zamu huku mpira ukichezwa zaidi katikati ya uwanja.
Advertisement
Dakika ya 79, Asha Rashid 'Mwalala' alitupatia bao la tatu baada ya kumalizia pasi ya Vivian Corazone na kukamilisha karamu ya mabao.
Kocha Musa Msosi alifanya mabadiliko ya kuwatoa, Coroline Rufa, Diana Mnally, Daniela Ngoyi, Jentrix Shikangwa na Ritticia Nabossa.
Na kuwaingiza, Gelwa Yonah, Doto Evarist, Esther Mayala, Asha Rashid na Danai Bhobho