Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na jambo zuri ni kuwa hakuna aliyepata majeruhi ambayo yatamfanya kukosa mchezo huo.
Morali ya wachezaji ipo juu na kila mmoja amejitahidi kuonyesha uwezo wake mazoezi ili kesho waaminiwe na kupata nafasi ya kuanza.
Advertisement
Pamoja na mambo mengine, tunaendelea kusisitiza mashabiki wawahi kufika mapema uwanjani ili kuepusha usumbufu kwa kuwa mchezo utaanza saa 10 jioni.