Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zote zikicheza mpira wa nguvu na kutengeneza nafasi lakini hawakuweza kuzitumia.
Mlinda mlango wa JKT, Omari Gonzo aliokoa shuti kali lililopigwa na Joshua Mutale dakika ya 36 ambalo lingeweza kutupa nafasi ya bao la kuongoza.
Mshambuliaji Edward Songo aliipatia JKT bao la kwanza dakika ya 60 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Paul Peter.
Mlinzi wa kati Wilson Nangu alitupatia bao la kusawazisha dakika ya 63 kwa kichwa baada ya mpira wa krosi uliopigwa na Elie Mpanzu.
Jonathan Sowah alitupatia bao la pili dakika ya 76 baada ya walinzi wa JKT kushindwa kuudhibiti mpira uliopigwa na Morice Abraham.
Ushindi huu umetufanya kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu baada ya kufikisha alama tisa kufuatia kushinda mechi zote tatu za mwanzo.
X1: Gonzo, Wahab (Kapalata 70'), Msengi, Paschal, Roony (Salum 58') Bajana (Makame 70') Nassor, Kilemile, Najimu (Songo 58') Paul, Dilunga
Waliionyeshwa kadi: Najimu 26' Gonzo 50' Wahabi 54' Kilemile 84'
X1: Yakoub, Kapombe, Mligo, Nangu, De Reuck, Kagoma (Kante 61'), Kibu (Mpanzu 61'), Naby, Mukwala (Sowah 61') Maema (Morice 61') Mutale (Jean Charles Ahoua)
Waliionyeshwa kadi: Kante 72'