Simba Sports Club
News

Tumefanikiwa kupata pointi tatu kwa Namungo

16 Nov 2022

Mchezo ulianza kwa kasi timu zote zikishambuliana kwa zamu kutafuta bao la mapema huku tukifika zaidi langoni kwao lakini tulipoteza nafasi.

Moses Phiri alitupatia bao hilo pekee dakika ya 33 baada ya shuti lililopigwa na Mohamed Hussein kupanguliwa na mlinda mlango wa Namungo, Deogratius Munish 'Dida' kabla ya kumkuta mfungaji.

Advertisement

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kuliandama lango la Namungo ambao muda mwingi walikuwa wakizuia na kufanya mashambulizi machache.

Kocha Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya mchezaji mmoja ambapo alimtoa Augustine Okrah na kumuingiza Victor Akpan.

Back to homepage
Share this story