Libasse Gueye alitupatia bao la kwanza dakika ya 11 akiwa ndani ya sita baada ya kupokea pasi kutoka kwa Anthony Mligo.
Anicet Oura alitupatia bao la pili dakika ya 26 kwa shuti kali la chini chini la mguu wa kulia baada ya kumzidi ujanja mchezaji wa Namungo kutoka katikati ya uwanja.
Heritier Makambo aliipatia Namungo bao la kwanza dakika ya 33 kwa mkwaju wa penati baada ya kiungo Yusuph Kagoma kuushika mpira ndani ya 18.
Elie Mpanzu alitupatia bao la tatu dakika ya 74 kwa shuti kali la mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Oura.
Ushindi huu unatufanya kufikisha alama 42 baada ya kucheza mechi 18 tukiwa nafasi ya pili kwenye msimamo.
Ligi Kuu ya NBC imesimama kupisha michuano ya Kombe la Muungano itakayofanyika Visiwani Zanzibar kuanzia Jumanne Aprili 21.
X1: Mussa, Jigwa (Kipenye 71') Machela, Kazi, Mgunya, Masawe (Kikoti 82'), Kiswanya, Nyenye, Makambo (Fabrice 61') Godfrey, Manyanya
Waliionyeshwa kadi: Rogers 68'
X1: Kassali, Kapombe, Mligo, Toure, De Reuck, Kagoma, Gueye (Kibaila 82'), Loemba (Maema 61'), Mwalimu (Mpanzu 61'), Chama (Morice 82'), Oura (Semfuko 87')
Waliionyeshwa kadi: Oura 61'