Simba Sports Club
News

Tumechukua Pointi tatu za Kagera

22 Jun 2025

Steven Mukwala alitupatia bao hilo pekee dakika ya 16 akiwa ndani ya 18 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na David Kameta 'Duchu'.

Baada ya bao hilo tukiendelea kufanya mashambulizi huku Kagera nao wakifanya yakushtukiza lakini hata hivyo hakuna aliyepata bao.

Kipindi cha pili tulipunguza kasi ya mchezo huku tukifika zaidi langoni mwa Kagera ingawa nafasi tulizopata tukishindwa kuzitumia.

Matokeo haya yanatufanya kufikisha pointi 78 tukiendelea kusalia nafasi ya pili huku tukiwa nyuma kwa alama moja.

Advertisement

X1: Camara, Duchu, Nouma, Chamou (Zimbwe Jr 82'), Che Malone, Ngoma (Okajepha 58'), Chasambi (Kapombe 77') Debora, Mukwala (Kibu 58'), Ahoua (Mutale 58') Awesu

Waliionyeshwa kadi: Debora 68'

X1: Kipao, Datus, Swedi, Mfuko, Mussa, Onditi, Siwa, Mahundi (Lookman 88') Amza, Fekha, Sigela

Waliionyeshwa kadi: Onditi 69' Mussa 90+3'

Back to homepage
Share this story