Simba Sports Club
News

Tumechukua alama zote za Mashujaa KMC Complex

2 May 2025

Mshambuliaji Jafar Kibaya aliipatia Mashujaa bao la mapema dakika ya sita kwa shuti kali la nje ya 18 baada ya kumzidi ujanja mlinzi Karabou Chamou.

Baada ya kufungwa bao hilo tuliongeza kasi ya kushambulia kutaka kusawazisha lakini Mashujaa walikuwa imara kuhakikisha wanazuia.

Leonel Ateba alitupatia bao la kusawazisha dakika ya 65 kwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi Mpoki Mwakinyuke kuunawa mpira wa krosi uliopigwa na Mohamed Hussein akiwa ndani ya 18.

Mlinda mlango wa Mashujaa, Patrick Muntari alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 80 baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kwa kosa la kupoteza muda.

Ateba alitupatia bao la pili kwa mkwaju wa penati tena dakika ya mwisho ya nyongeza baada ya mlinzi Shomari Kapombe kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Advertisement

X1: Camara, Duchu (Kapombe 45'), Nouma (Zimbwe Jr 45'), Chamou, Hamza, Kagoma, Balua (Kibu 45'), Debora (Mukwala 82'), Ateba, Awesu (Mutale 61'), Mpanzu,

Waliionyeshwa kadi:

X1: Muntari, Mbegu (Ngushi 60'), Mwakinyuke, Mtuwi, Abdulmalik, Dunia, Munthir (Martin 75'), Stambuli, Kibaya (Lyanga 57'), Balama (Cheda 75'), Gamal

Waliionyeshwa kadi: Muntari 50' Ngushi 90+17

Back to homepage
Share this story