Seleman Mwalimu alitupatia bao la kwanza kwa mkwaju wa penati dakika ya 11 baada ya Nickson Kibabage kufanyiwa madhambi na mlinzi Nasri Kombo ndani ya 18.
Baada ya bao hilo tuliendelea kutengeneza nafasi huku TRA nao wakijaribu mara kadhaa kuja langoni kwetu lakini tulikuwa imara kuwakabili.
Neo Maema alitupatia bao la pili dakika ya 66 kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja nje kidogo ya 18 baada ya Libasse Gueye kufanyiwa madhambi na Joseph Akandwanaho.
Yusuph Kagoma alitupatia bao la tatu kwa kichwa dakika ya 89 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Elie Mpanzu.
X1: Kassali, Kapombe Kibabage Toure, De Reuck Kagoma (Semfuko 90'), Gueye (Kante 70'), Maema (Morice 70'), Mwalimu (Mpanzu 70'), Chama (Kibaila 87'), Oura.
Ushindi huu unatufanya kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo tukiwa na alama 31 baada ya kucheza mechi 14.
Waliionyeshwa kadi: Morice 90+3'
X1:Noel, Chobwedo (Jiah 82'), Kombo, Tibandeke, Joseph, Mapaka, Nkane, Jamal, Omary.(Makoye 59'), Lazarus (Emmanuel 87'), Chewe (Pamba 59')
Waliionyeshwa kadi: Akandwanaho 65'