Simba Sports Club
News

Tumechukua alama tatu za Coastal

2 Apr 2026

Seleman Mwalimu alitupatia bao la kwanza dakika ya 25 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Clatous Chama na kumpiga chenga mlinda mlango Chuma Mgeni kabla ya kufunga.

Baada ya hilo tuliendelea kutengeneza nafasi na kulifikia zaidi lango la Coastal ambao walikuwa nyuma muda mwingi na kufanya mashambulizi ya kushtukiza.

Mlinzi Ismail Toure alitupatia bao la pili dakika ya 45 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Neo Maema.

Kipindi cha pili tulipunguza kasi huku kocha Steve Barker akifanya mabadiliko ya wachezaji mara kwa mara ambapo tuliwapa nafasi Coastal kufika langoni kwetu mara kadhaa.

Ushindi huu unatufanya kufikisha alama 34 tukipanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 15.

Advertisement

X1: Abel, Kapombe (Duchu 74'), Kibabage (Mligo 45'), Toure, De Reuck, Kante (Semfuko 60'), Gueye, Maema, Mwalimu, Chama (Abraham 60'), Oura (Chasambi 79')

Waliionyeshwa kadi: Maema 90+1'

X1: Chuma, Gofrey, Ally, Maabad ( Segeja 45') Gradi, Greyson (Mwanza 79') Bakari, Abdallah, Shiza (Andrew 66'), Aidan, Yassin (Nasser 66')

Waliionyeshwa kadi: Gradi 55' Gwalala 56'

Back to homepage
Share this story