Simba Sports Club
News

Tumechukua alama tatu Lake Tanganyika

1 Nov 2024

Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zikishambuliana kwa zamu lakini sisi tulifika zaidi langoni mwa Mashujaa.

Mlinda mlango wa Mashujaa Eric Johora alikuwa shujaa kwa timu hiyo kipindi cha kwanza baada kuokoa michomo miwili ya adhabu iliyopigwa na Kibu Denis.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi hasa baada ya kuwaingiza Jean Charles Ahoua na Debora Fernandes.

Mshambuliaji Steven Mukwala alitupatia bao pekee kwa kichwa dakika ya mwisho ya nyongeza baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Awesu Awesu.

Matokeo haya yametufanya kufikisha alama 22 tukipanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo.

Advertisement

X1: Johora, Gamal, Mwakinyuke, Mtuwi, Abdulmalik (Protas 54'), Dunia, Stambuli, Cheda, Mgunda, Balama, Karihe

Walioonyeshwa kadi: Johora 84'

X1: Camara, Kapombe, Zimbwe Jr (Nouma 81'), Che Malone, Chamou, Ngoma (Mukwala 63'), Mutale (Fernandez 45'), Okajepha, Ateba (Awesu 71'), Kibu, Ladaki (Ahoua 45')

Walioonyeshwa: Okajepha 68'

Back to homepage
Share this story