Simba Sports Club
News

Tumeanza vizuri mzunguko wa pili NBC

4 Mar 2022

Pape Sakho alitupatia bao la kwanza dakika ya nane kwa shuti kali ndani ya 18 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Shomari Kapombe kutoka upande wa kulia.

Dakika ya 13 Mzamiru Yassin alitupatia bao la pili kwa kichwa akimalizia mpira krosi uliopigwa kwa ustadi na Kapombe.

Clatous Chama alitupatia bao la tatu dakika ya 18 baada ya kuwalamba chenga walinzi wawili wa Biashara Boniface Maganga na Abdulamajid Mangalo kufuatia pasi safi ya Sakho.

Kapombe alishindwa kuendelea na mchezo na kutolewa dakika ya 28 baada ya kugongwa kichwani na mshambuliaji Atupele Green.

Advertisement

Kipindi cha pili tulitengeneza nafasi nyingi huku tukifanya mashambulizi lakini hata hivyo ufanisi wetu kwenye kuzitumia haukuwa wa kutosha.

Dakika ya 92 Medie Kagere alikosa mkwaju wa penati uliodakwa na mlinda mlango wa Biashara James Ssetuba baada ya Bernard Morrison kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Kocha Pablo Franco aliwatoa John Bocco, Sakho, Mohamed Hussein, Henock Inonga na kuwaingiza Kagere, Morrison, Gadiel Michael na Kennedy Juma.

Back to homepage
Share this story