Simba Sports Club
News

Tumeanza na Ushindi michuano ya Mapinduzi

3 Jan 2026

Mohamed Bajaber alitupatia bao hilo dakika ya 21 akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Neo Maema.

Baada ya bao hilo tuliendelea kutengeneza nafasi huku tukilifikia zaidi lango la Mwembe Makumbi lakini walikuwa imara kuondoa hatari.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi ya kutafuta bao la pili lakini hata hivyo tulikosa njia ya kupenya safu ya ulinzi ya Mwembe Makumbi ambayo ilikuwa imara muda wote.

Advertisement

Kikosi chetu kitashuka tena dimbani Jumatatu, Januari 5 kuikabili Fufuni katika mchezo wa pili wa michuano hii.

X1: Abel, Duchu, Mligo, Chamou, De Reuck (Masinde 71') Semfuko (Awesu 78') Chasambi (Mzamiru 71') Naby, Mwangosi, Maema (Bashiru 60'), Bajaber (Mutale 60')

Back to homepage
Share this story