Tumepangwa na Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya droo kukamilika leo jioni Cairo, nchini Misri.
Miamba hii tulikutana nayo katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Deesemba 30, mwaka 2019 nchini Afrika Kusini na kumalizika kwa sare ya bao moja.
Advertisement
Kikosi chetu wakati huo kilikuwa chini ya Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems ambapo bao letu lilifungwa na kiungo mshambuliaji, Clatous Chama.
Mchezo wetu dhidi ya Orlando inategemewa kuwa mkali kutokana na ubora wa timu zote na aina ya uchezaji.