Simba Sports Club
News

Try Again: Safari ya Mafanikio lazima iwe na Changamoto

15 Nov 2023

Try Again amesema miaka ya nyuma tulikuwa tunatolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa kwa idadi kubwa ya mabao ikaja kutolewa kwa mikwaju ya penati mpaka sasa tumetolewa kwa kanuni ya bao la ugenini.

Try Again amesema kujenga timu ni mchakato mrefu sio wa usiku mmoja kwa hiyo mashabiki wawe na subira viongozi wanapambana usiku na mchana kuhakikisha tunakuwa na kikosi imara.

"Simba ni miongoni mwa timu bora Afrika kwa sasa, ukiangalia katika mechi za michuano ya Ligi ya Mabingwa huko nyuma tulikuwa tunatolewa kwa kufungwa mabao mengi.

Advertisement

"TP Mazembe walitufunga mabao manne, Al Ahly walitufunga matano lakini Kaizer Chiefs na Wydad Casablanca walitutoa kwa penati na juzi kwenye African Football League Al Ahly wametutoa kwa kanuni ya bao la ugenini," amesema Try Again.

Try Again ameendelea kusema kuwa "mashabiki wetu waendelee kuipa sapoti timu sababu safari ya mafanikio ina changamoto nyingi, baada ya muda mfupi tutarejea kwenye furaha yetu," amesema Try Again.

Back to homepage
Share this story