Kikosi kimeondoka jijini Dar es Salaam mchana na baada ya kufika wachezaji walipumzika kabla ya usiku kuelekea uwanjani kwa ajili ya mazoezi tayari kwa maandalizi ya mtanange wa kesho.
Wachezaji wote 20 tuliosafiri nao wameshiriki mazoezi hayo na wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho.
Advertisement
Mchezo wetu dhidi ya JKU utapigwa kesho saa 2:15 usiku katika Uwanja wa New Amaan Complex.