Kikosi kimeondoka jijini Dar es Salaam jioni kikiwa na wachezaji 21, benchi la ufundi pamoja na baadhi ya viongozi.
Jumapili saa 2:15 usiku kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Amani kucheza na Malindi katika mchezo wa kwanza wa kirafiki.
Advertisement
Jumatano Septemba, 28 tutacheza mchezo wa pili wa kirafiki dhidi ya Kipanga FC katika Uwanja huo huo wa Amani saa 2:15 usiku.
Kesho timu itafanya mazoezi ya mwisho kujiandaa na Malindi kabla ya kushuka dimbani Jumapili.