Simba Sports Club
News

Timu yawasili salama Uganda

23 Feb 2023

Kesho kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa St. Mary's ambapo mchezo wetu utapigwa siku ya Jumamosi.

Hali ya wachezaji ni nzuri na morali ipo juu na kila mmoja yupo tayari kuhakikisha anapambana kuipigania timu kupata ushindi dhidi ya Vipers.

Advertisement

Mchezo wetu dhidi ya Vipers utapigwa Jumamosi katika Uwanja wa St. Mary's wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 15,000 kuanzia saa moja usiku.

Back to homepage
Share this story