Simba Sports Club
News

Timu yawasili salama Tunisia

1 Jan 2025

Kikosi kimeondoka jijini Dar es Salaam alfajiri ya leo kikipitia Instanbul, Uturuki kabla ya kuunganisha Ndege kuelekea Tunisia.

Timu imeondoka na msafara wa watu 50 huku wachezaji wakiwa 22 ambao tunaamini wapo tayari kuipambania timu kupata matokeo chanya.

Advertisement

Kikiwa hapa Tunisia kikosi chetu kitapata nafasi ya kufanya mazoezi kwa siku tatu huku kikizoea hali ya hewa.

Mchezo huo ambao utapigwa Januari 5 saa moja usiku kwa saa za Tanzania hautakuwa na mashabiki.

Back to homepage
Share this story