Simba Sports Club
News

Timu yawasili salama Libya

12 Sep 2024

Kikosi kimeondoka Uturuki asubuhi na kuelekea Libya kufuatia safari ya jana ya kutokea jijini Dar es Salaam.

Wachezaji waliokuwa kwenye majukumu ya timu za Taifa Ally Salim Mohamed Hussein, Edwin Balua na Moussa Camara tayari wamejiunga na wenzao.

Advertisement

Baada ya kuwasili Libya wachezaji watapata saa chache za kupumzika na jioni wataanza programu ya mazoezi.

Tutakuwa na siku tatu za kufanya mazoezi nchini Libya kabla ya kukutana na Al Ahly Tripoli ili kuwafanya wachezaji wetu kuzoea hali ya hewa.

Back to homepage
Share this story