Kikosi kimefika katika mji wa Conakry ambapo mchezo wetu wa Jumamosi utafanyika saa 10 jioni kwa saa Guinea ambapo nyumbani itakuwa itakuwa saa moja usiku.
Wachezaji wote 24 waliosafiri wapo sawa kiafya ukiacha uchovu wa safari ndefu angani lakini wapo kamili kuipigania Simba.
Advertisement
Kesho kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa (Stade General Lansana Conte) ambao utatumika kwa mechi kwa mujibu wa kanuni za CAF ili kujiweka sawa kwa pambano la Jumamosi.