Kikosi kiliondoka asubuhi jijini Dar es Salaam kwa Ndege ya Air Tanzania kikipitia Afrika Kusini kabla ya kuunganisha mpaka Eswatini.
Baada ya kuwasili Eswatini kesho kikosi kitafanyika mazoezi ya utimamu wa mwili na Jumamosi watafanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Somhololo kabla ya kushuka dimbani Jumapili.
Advertisement
Wachezaji wote 22 tuliosafiri nao kwa ajili ya mchezo huo wapo kwenye hali nzuri na tayari kwa mchezo ambao malengo yetu ni kupata matokeo chanya.