Baada ya kuwasili wachezaji wamepewa mapumziko ya saa chache na leo jioni kikosi kitaendelea na mazoezi katika kujiandaa na mchezo wa tatu dhidi ya CS Sfaxien kutoka Tunisia.
Mchezo dhidi ya CS Sfaxien utapigwa Jumapili katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni ambao tunatarajia utakuwa mgumu.
Advertisement
Malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda mechi zote za nyumbani ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya robo fainali.