Tumesafiri na kikosi kamili cha wachezaji 24 na tunatarajia kufanya mazoezi ya utimamu wa mwili jioni.
Tumesafiri na kikosi kamili kwakuwa tutakuwa na mechi tatu za Kanda ya Ziwa dhidi ya Geita, Kagera Sugar na KMC kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam.
Advertisement
Dhamira yetu ni kuhakikisha tunashinda mechi zote tatu ingawa tunajua haitakuwa kazi rahisi kwakuwa tunaingia katika mzunguko wa pili na kila timu inapambana kutafuta alama ili kujiweka kwenye nafasi nzuri.