Simba Sports Club
News

Timu yatua Dar, kuanza maandalizi ASFC

27 Jan 2022

Kikosi kimerejea jijini Dar es Salaam salama kutoka mkoani Kagera na moja kwa moja kinaanza maandalizi ya mchezo wa Azam Sports Federation Cup (ASFC) hatua ya 32 bora.

Jumapili Januari 30 saa moja usiku kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Dar City katika michuno hiyo.

Advertisement

Licha ya kutokuwa na muda wa kutosha wa kupumzika kutokana na ratiba kuwa ngumu lakini tunajipanga kuhakikisha tunafanya vizuri.

Malengo yetu ni kuhakikisha tunatetea ubingwa wa michuano hiyo hivyo kila mchezo tunauchukulia kwa umakini mkubwa bila kuangalia tunacheza na nani.

Back to homepage
Share this story