Simba Sports Club
News

Timu yarejea, Zimbwe Jr atoa neno

18 Sep 2024

Zimbwe Jr amesema tunajua utakuwa mchezo mgumu kutokana na ubora wa Al Ahli Tripoli lakini tupo kwenye ardhi ya nyumbani tukiwa tunajua nyuma kuna mashabiki wetu.

Zimbwe amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu kwakuwa wana mchango mkubwa kutimiza malengo ya kuisaidia timu kufika hatua ya makundi.

"Tumerudi salama nyumbani, tukiwa na nguvu na ari ya kupambana kuhakikisha tunaibuka na ushindi na kutinga hatua ya makundi ya michuano hii."

Advertisement

"Al Ahli Tripoli ni timu bora na walitupa upinzani mkubwa pia walipata nguvu kubwa kutoka kwa mashabiki wao, nasi tunaamini Jumapili tutakuwa na mashabiki wetu hivyo tupo kwenye nafasi yakufanya vizuri," amesema Zimbwe Jr.

Kikosi chetu kimewasili alfajiri kutoka Libya kikipitia Uturuki kabla ya kuwasili nchini na moja kwa moja kimeingia kambini kujiandaa na mchezo huo.

Back to homepage
Share this story