Simba Sports Club
News

Timu yarejea salama Dar es Salaam

10 Mar 2024

Kikosi kimeondoka Tanga mchana baada ya kufanya mazoezi ya utimamu wa mwili ili kuwaweka wachezaji sawa kabla ya kuanza safari.

Baada ya kufika wachezaji wameruhusiwa kwenda kupumzika na kesho mchana kikosi kitaingia kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Singida Fountain Gate utakaopigwa Jumanne saa moja usiku Uwanja wa Azam Complex.

Advertisement

Kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena tayari kwa kuwavaa Singida.

Back to homepage
Share this story