Simba Sports Club
News

Timu yarejea nyumbani salama

1 Mar 2022 By simbasc 837 views

Kikosi chetu kimewasili salama jijini Dar es Salaam leo mchana kutoka nchini Morocco baada ya majukumu ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi kukamilika.

Baada ya kufika Dar wachezaji wameruhusiwa kwenda kuziona familia zao na kesho watarajea mazoezini kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu ya NBC itakayopigwa Ijumaa Machi 4, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku dhidi ya Biashara United.

Advertisement

Mechi hiyo ni muelendelezo wa ligi ambapo tutakuwa tunaanza rasmi mzunguko wa pili.

Katika mchezo huo tunatarajia uwepo wa baadhi ya wachezaji wetu ambao walikuwa majeruhi na kuikosa mechi kadhaa ambao watakuwa wamepona na wako fiti.

Back to homepage
Share this story