Simba Sports Club
News

Timu yarejea mazoezini

17 May 2023

Mazoezi hayo yamefanyika katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena chini ya kocha mkuu Roberto Oliveira 'Robertinho' na wasaidizi wake.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri kujiandaa na mechi zilizobaki.

Advertisement

Mchezo wetu unaofuata utakuwa dhidi ya Polisi Tanzania ambao ulisogezwa mbele lakini bado haujapangiwa tarehe ya kuchezwa.

Tunaamini mchezo huo utapigwa wiki ijayo ndio maana kikosi kimerejea mazoezini kujiandaa ili tarehe itakapotangazwa tuwe tayari.

Back to homepage
Share this story