Simba Sports Club
News

Timu yarejea mazoezini Mo Arena

7 Oct 2025

Mazoezi hayo ambayo yatafanyika saa 10 jioni katika Uwanja wa Mo Simba Arena yataongozwa na Meneja mkuu Dimitar Pantev pamoja na wasaidizi wake wa benchi la ufundi.

Wachezaji waliopo kwenye majukumu ya timu za Taifa wameruhusiwa kwenda kujiunga na timu zao na watarejea mara tu watakapomaliza.

Advertisement

Wachezaji waliopo kwenye majukumu ya timu za Taifa ya Tanzania ni Yakoub Suleiman, Shomari Kapombe, Yusuph Kagoma, Morice Abraham na Seleman Mwalimu.

Wengine walioitwa ni mshambuliaji Steven Mukwala (Uganda 'The Cranes') na mlinda mlango Moussa Camara (Mali).

Back to homepage
Share this story