Simba Sports Club
News

Timu yarejea mazoezini kujiandaa na Wydad

16 Dec 2023 By simbasc 608 views
Kikosi chetu kimefanya mazoezi katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca utakaopigwa Jumanne saa 10 jioni katika Uwanja wa Azam Complex. Baada ya ushindi wa jana dhidi ya Kagera Sugar leo kikosi kimeendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo huo ambao tunahitaji alama tatu kwa kila hali. Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu na wapo kwenye hali na morali zikiwa juu hasa zikichagizwa na ushindi tuliopata jana. Katika mchezo dhidi ya Wydad tutawakosa nyota wetu wawili Sadio Kanoute na Said Ntibazonkiza kwakuwa wanatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.
Advertisement
Back to homepage
Share this story