Wachezaji walipewa mapumziko ya siku taru baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union tulioibuka na ushindi wa mabao 3-0 tuliocheza Alhamisi na leo tumeanza rasmi mawindo ya Power Dynamos.
Wachezaji wameshiriki kikamilifu mazoezi hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Mo Simba Arena na wamejitahidi kufuata maelekezo kwa umakini waliyokuwa wanapewa na makocha.
Advertisement
Morali za wachezaji zipo juu na kila mmoja amejitahidi kuonyesha uwezo wake ili kulishawishi benchi la ufundi kumpa nafasi siku ya Jumapili.
Programu ya mazoezi itaendelea kesho chini ya kocha mkuu, Roberto Oliviera 'Robertinho' na wasaidizi wake wa benchi la ufundi.