Mchezo wetu dhidi ya Jwaneng utapigwa katika Uwanja wa Obed Itani Chilume kwenye mji wa Francistown saa 10 jioni kwa saa za nyumbani Tanzania.
Tunajua umuhimu wa kupata pointi tatu kwenye mchezo huo ingawa tunajua utakuwa mgumu lakini tupo tayari kupambana.