Kabla ya kuanza safari ya kurejea Dar es Salaam kikosi kimefanya mazoezi ya utimamu wa mwili ili kuondoa uchovu wa mechi.
Kesho Kikosi kitaanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo unaofuata wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Oktoba 4 katika Uwanja wa KMC Complex saa 10:15 jioni.