Baada ya kikosi kufika wachezaji wamepewa mapumziko na kesho watarejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa ligi unaofuata dhidi ya Ihefu FC.
Mchezo wetu dhidi ya Ihefu utapigwa Jumamosi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.
Advertisement
Tutakuwa na siku mbili za kujiandaa na mchezo dhidi ya Ihefu lakini tunaamini maandalizi yetu yatatufanya kupata matokeo chanya.