Baada ya kikosi kurejea asubuhi ya leo na kuingia kambini na jioni kitafanya mazoezi katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo huo ambao tunategemea utakuwa mgumu.
Jana tulikuwa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Pamba Jiji uliopigwa Uwanja wa CCM Kirumba na kumalizika kwa sare ya kufungana bao moja.
Advertisement
Jambo la kumshukuru Mungu kwenye mchezo wa jana hatukupata mchezaji aliyepata majeraha hivyo wote wataanza mazoezi kujiandaa na TRA jioni.
Mchezo wetu dhidi ya TRA United utapigwa Jumapili katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo saa moja usiku.