Baada ya kufika wachezaji wamepewa mapumziko na kesho wataanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Ijumaa, Disemba 15 jijini Dar es Salaam.
Pamoja na uchovu kutokana na umbali wa safari kutoka Morocco wachezaji hawajapewa muda mwingi wa kupumzika kwakuwa tuna ratiba ngumu iliyopo mbele yetu.
Advertisement
Baada ya mechi dhidi ya Kagera siku ya Ijumaa siku tatu baadae tutakuwa na mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca.