Simba Sports Club
News

Timu yarejea Dar, Wachezaji wapewa mapumziko

23 Jan 2023 By simba 240 views
  Kikosi kimerejea mchana jijini Dar es Salaam kutoka Dodoma baada ya ushindi wa bao moja tuliopata jana dhidi ya Dodoma Jiji. Baada ya kufika wachezaji wamepewa mapumziko na kesho kikosi kitarejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Jumamosi, Benjamin Mkapa. Mazoezi hayo yatafanyika saa 10 jioni katika Uwanja wa Mo Simba Arena ambapo wachezaji wote wanatarajiwa kuhudhuria. Lengo letu ni kuhakikisha tunachukua ubingwa wa michuano hii na tunapaswa kushinda kila mchezo tukianza na Coastal, Jumamosi.
Advertisement
Back to homepage
Share this story